Mt. 2:17-23 Swahili Union Version (SUV)

17. Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,

18. Sauti ilisikiwa Rama,Kilio, na maombolezo mengi,Raheli akiwalilia watoto wake,Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.

19. Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri,

20. akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.

21. Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli.

22. Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya,

23. akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.

Mt. 2