26. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
27. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.
28. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho.
29. Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
30. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.
31. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.
32. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;
33. nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?