Mt. 18:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,

2. Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,

3. akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

4. Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.

5. Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;

6. bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.

Mt. 18