6. basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
7. Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
8. Watu hawa huniheshimu kwa midomo;Ila mioyo yao iko mbali nami.
9. Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundishoYaliyo maagizo ya wanadamu.
10. Akawaita makutano akawaambia
11. Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
12. Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?
13. Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.
14. Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.
15. Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.
16. Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
17. Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?