1. Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema,
2. Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.
3. Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
4. Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.
5. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,
6. basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
7. Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
8. Watu hawa huniheshimu kwa midomo;Ila mioyo yao iko mbali nami.
9. Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundishoYaliyo maagizo ya wanadamu.