Mt. 14:8-14 Swahili Union Version (SUV)

8. Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.

9. Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe;

10. akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.

11. Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye.

12. Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.

13. Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao.

14. Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.

Mt. 14