31. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?
32. Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma.
33. Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.
34. Na walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti.
35. Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi;
36. nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa kabisa.