Mt. 14:10-25 Swahili Union Version (SUV)

10. akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.

11. Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye.

12. Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.

13. Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao.

14. Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.

15. Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.

16. Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula.

17. Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili.

18. Akasema, Nileteeni hapa.

19. Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.

20. Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.

21. Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.

22. Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.

23. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.

24. Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.

25. Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.

Mt. 14