Mt. 13:4-13 Swahili Union Version (SUV)

4. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;

5. nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina;

6. na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.

7. Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;

8. nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.

9. Mwenye masikio na asikie.

10. Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?

11. Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.

12. Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

13. Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.

Mt. 13