Mt. 13:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari.

2. Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.

3. Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.

Mt. 13