Mt. 13:1-10 Swahili Union Version (SUV)

1. Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari.

2. Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.

3. Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.

4. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;

5. nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina;

6. na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.

7. Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;

8. nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.

9. Mwenye masikio na asikie.

10. Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?

Mt. 13