14. Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.
15. Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,
16. akawakataza wasimdhihirishe;
17. ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
18. Tazama, mtumishi wangu niliyemteua;Mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye;Nitatia roho yangu juu yake,Naye atawatangazia Mataifa hukumu.
19. Hatateta wala hatapaza sauti yake;Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.
20. Mwanzi uliopondeka hatauvunja,Wala utambi utokao moshi hatauzima,Hata ailetapo hukumu ikashinda.
21. Na jina lake Mataifa watalitumainia.