Mt. 12:10-18 Swahili Union Version (SUV)

10. Na tazama, yumo mtu mwenye mkono umepooza; wakamwuliza, wakisema, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? Wapate kumshitaki.

11. Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwopoa?

12. Je! Mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi? Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato.

13. Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, ukawa mzima kama wa pili.

14. Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.

15. Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,

16. akawakataza wasimdhihirishe;

17. ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,

18. Tazama, mtumishi wangu niliyemteua;Mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye;Nitatia roho yangu juu yake,Naye atawatangazia Mataifa hukumu.

Mt. 12