Mt. 11:3-8 Swahili Union Version (SUV)

3. Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

4. Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona;

5. vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.

6. Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.

7. Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?

8. Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme.

Mt. 11