10. Huyo ndiye aliyeandikiwa haya,Tazama, mimi namtuma mjumbe wanguMbele ya uso wako,Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.
11. Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.
12. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
15. Mwenye masikio, na asikie.
16. Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema,
17. Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.
18. Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
19. Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
20. Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.
21. Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.
22. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.