Mt. 11:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

2. Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,

3. Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

Mt. 11