Mt. 10:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.

2. Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya; Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye;

3. Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo;

4. Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote, naye ndiye mwenye kumsaliti.

5. Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie.

6. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

7. Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.

8. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

9. Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;

Mt. 10