4. Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani?
5. Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba,
6. Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano.
7. Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia.
8. Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.
9. Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga.
10. Mara akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda pande za Dalmanutha.
11. Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu.