Mk. 8:28-30 Swahili Union Version (SUV)

28. Wakamjibu, Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; wengine, Mmojawapo wa manabii.

29. Naye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo.

30. Akawaonya wasimwambie mtu habari zake.

Mk. 8