34. akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.
35. Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.
36. Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari;
37. wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.