3. Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao;
4. tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.
5. Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi?
6. Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa,Watu hawa huniheshimu kwa midomoIla mioyo yao iko mbali nami;
7. Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundishoYaliyo maagizo ya wanadamu,
8. Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.
9. Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.
10. Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe.
11. Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;