Mk. 6:50-56 Swahili Union Version (SUV)

50. kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.

51. Akapanda mle chomboni walimo; upepo ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao;

52. kwa maana hawakufahamu habari za ile mikate, lakini mioyo yao ilikuwa mizito.

53. Hata walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.

54. Nao wakiisha kutoka mashuani, mara watu walimtambua,

55. wakaenda mbio, wakizunguka nchi ile yote, wakaanza kuwachukua vitandani walio hawawezi, kwenda kila mahali waliposikia kwamba yupo.

56. Na kila alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse ngaa pindo la vazi lake; nao wote waliomgusa wakapon

Mk. 6