47. Na kulipokuwa jioni mashua ilikuwa katikati ya bahari, na yeye yu peke yake katika nchi kavu.
48. Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita.
49. Nao walipomwona anatembea juu ya bahari, walidhani ya kuwa ni kivuli, wakapiga yowe,
50. kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.
51. Akapanda mle chomboni walimo; upepo ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao;
52. kwa maana hawakufahamu habari za ile mikate, lakini mioyo yao ilikuwa mizito.
53. Hata walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.