12. ili wakitazama watazame, wasione;Na wakisikia wasikie, wasielewe;Wasije wakaongoka, na kusamehewa.
13. Akawaambia, Hamjui mfano huu? Basi mifano yote mtaitambuaje?
14. Mpanzi huyo hulipanda neno.
15. Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.
16. Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha;