Mk. 3:23-34 Swahili Union Version (SUV)

23. Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani?

24. Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;

25. na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.

26. Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo.

27. Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.

28. Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;

29. bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,

30. kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu.

31. Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita.

32. Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka, wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.

33. Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?

34. Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu!

Mk. 3