20. Mkutano wakakusanyika tena, hata wao wenyewe wasiweze hata kula mkate.
21. Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.
22. Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.
23. Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani?
24. Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;
25. na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
26. Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo.
27. Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.
28. Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;
29. bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,
30. kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu.
31. Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita.