2. wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.
3. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.
4. Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.
5. Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
6. Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza.
7. Naye Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Mkutano mkuu ukamfuata, kutoka Galilaya, na Uyahudi,
8. na Yerusalemu, na Idumaya, na ng’ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.
9. Akawaambia wanafunzi wake ya kwamba chombo kidogo kikae karibu naye, kwa sababu ya mkutano, wasije wakamsonga.
10. Maana aliponya wengi, hata wote waliokuwa na misiba wakamrukia wapate kumgusa.
11. Na pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.
12. Akawakataza sana, wasimdhihirishe.
13. Akapanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea.
14. Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri,