14. Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri,
15. tena wawe na amri ya kutoa pepo.
16. Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro;
17. na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo;
18. na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,
19. na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.Kisha akaingia nyumbani.
20. Mkutano wakakusanyika tena, hata wao wenyewe wasiweze hata kula mkate.