1. Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;
2. wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.
3. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.
4. Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.