Mk. 2:22-24 Swahili Union Version (SUV)

22. Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya.

23. Ikawa alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato, wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke.

24. Mafarisayo wakamwambia, Tazama, mbona wanafanya lisilokuwa halali siku ya sabato?

Mk. 2