23. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele.
24. Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake.
25. na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.
26. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.
27. Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu.
28. Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu;
29. nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni.
30. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie.
31. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
32. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.