Mk. 12:21-24 Swahili Union Version (SUV)

21. Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Na wa tatu kadhalika;

22. hata na wote saba, wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.

23. Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye.

24. Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?

Mk. 12