Mk. 11:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Hata walipokaribia Yerusalemu karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, aliwatuma wawili katika wanafunzi wake,

2. akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.

3. Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji na mara atamrudisha tena hapa.

4. Wakaenda zao, wakamwona mwana-punda amefungwa penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua.

5. Baadhi ya watu waliosimama huko wakawaambia, Mnafanya nini kumfungua mwana-punda?

6. Wakawaambia kama Yesu alivyowaagiza, nao wakawaruhusu.

7. Wakamletea Yesu yule mwana-punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake.

8. Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani.

9. Nao watu waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti, Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana;

Mk. 11