Mk. 1:40-44 Swahili Union Version (SUV)

40. Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.

41. Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.

42. Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.

43. Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara,

44. akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.

Mk. 1