Mk. 1:32-43 Swahili Union Version (SUV)

32. Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo.

33. Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni.

34. Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.

35. Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.

36. Simoni na wenziwe wakamfuata;

37. nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta.

38. Akawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea.

39. Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.

40. Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.

41. Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.

42. Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.

43. Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara,

Mk. 1