5. Njoo ule mkate wangu,Ukanywe divai niliyoichanganya.
6. Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi,Mkaende katika njia ya ufahamu.
7. Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha;Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.
8. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia;Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.
9. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima;Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
10. Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
11. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa;Na miaka ya maisha yako itaongezwa.
12. Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako;Na kama una dharau, utaichukua peke yako.
13. Mwanamke mpumbavu hupiga kelele,Ni mjinga, hajui kitu.