14. Hukaa mlangoni pa nyumba yake,Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka,
15. Apate kuwaita wapitao njiani,Waendao moja kwa moja katika njia zao.
16. Kila aliye mjinga na aingie humu.Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,
17. Maji yaliyoibiwa ni matamu,Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza.
18. Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo;Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni.