Mit. 9:1-11 Swahili Union Version (SUV)

1. Hekima umeijenga nyumba yake,Amezichonga nguzo zake saba;

2. Amechinja nyama zake, umechanganya divai yake,Ameiandalia meza yake pia.

3. Amewatuma wajakazi wake, analia,Mahali pa mjini palipoinuka sana,

4. Kila aliye mjinga na aingie humu.Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,

5. Njoo ule mkate wangu,Ukanywe divai niliyoichanganya.

6. Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi,Mkaende katika njia ya ufahamu.

7. Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha;Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.

8. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia;Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.

9. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima;Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;

10. Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

11. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa;Na miaka ya maisha yako itaongezwa.

Mit. 9