2. Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia,Penye njia panda, ndipo asimamapo.
3. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini,Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.
4. Enyi watu, nawaita ninyi;Na sauti yangu ni kwa wanadamu.
5. Enyi wajinga, fahamuni werevu,Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu.
6. Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri,Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili.
7. Maana kinywa changu kitasema kweli,Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu.
8. Maneno yote ya kinywa changu yana haki;Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.
9. Yote humwelea yule afahamuye,Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa.
10. Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,Na maarifa kuliko dhahabu safi.