Mit. 7:20-26 Swahili Union Version (SUV)

20. Amechukua mfuko wa fedha mkononi;Atarudi wakati wa mwezi mpevu.

21. Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi,Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.

22. Huyo akafuatana naye mara hiyo,Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni;Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;

23. Hata mshale umchome maini;Kama ndege aendaye haraka mtegoni;Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.

24. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.

25. Moyo wako usizielekee njia zake,Wala usipotee katika mapito yake.

26. Maana amewaangusha wengi waliojeruhi,Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.

Mit. 7