10. Na tazama, mwanamke akamkuta,Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;
11. Ana kelele, na ukaidi;Miguu yake haikai nyumbani mwake.
12. Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani,Naye huotea kwenye pembe za kila njia.
13. Basi akamshika, akambusu,Akamwambia kwa uso usio na haya,
14. Kwangu ziko sadaka za amani;Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu;
15. Ndiyo maana nikatoka nikulaki,Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona.
16. Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri,Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari.
17. Nimetia kitanda changu manukato,Manemane na udi na mdalasini.
18. Haya, na tushibe upendo hata asubuhi,Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba.