1. Mwanangu, yashike maneno yangu,Na kuziweka amri zangu akiba kwako.
2. Uzishike amri zangu ukaishi,Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.
3. Zifunge katika vidole vyako;Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4. Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu;Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke.
5. Wapate kukulinda na malaya,Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.
6. Maana katika dirisha la nyumba yanguNalichungulia katika shubaka yake;
7. Nikaona katikati ya wajinga,Nikamtambua miongoni mwa vijana,Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
8. Akipita njiani karibu na pembe yake,Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,
9. Wakati wa magharibi, wakati wa jioni,Usiku wa manane, gizani.
10. Na tazama, mwanamke akamkuta,Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;