Mit. 6:26-34 Swahili Union Version (SUV)

26. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate;Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani

27. Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake,Na nguo zake zisiteketezwe?

28. Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto,Na nyayo zake zisiungue?

29. Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake;Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.

30. Watu hawamdharau mwivi,Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;

31. Lakini akipatikana, atalipa mara saba;Atatoa mali yote ya nyumba yake.

32. Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

33. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;Wala fedheha yake haitafutika.

34. Maana wivu ni ghadhabu ya mtu;Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.

Mit. 6