Mit. 5:9-22 Swahili Union Version (SUV)

9. Usije ukawapa wengine heshima yako,Na wakorofi miaka yako;

10. Wageni wasije wakashiba nguvu zako;Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;

11. Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho,Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;

12. Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo,Na moyo wangu ukadharau kukemewa;

13. Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu,Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!

14. Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote,Katikati ya mkutano na kusanyiko.

15. Unywe maji ya birika lako mwenyewe,Na maji yenye kububujika katika kisima chako.

16. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali,Na mito ya maji katika njia kuu?

17. Yawe yako mwenyewe peke yako,Wala si ya wageni pamoja nawe.

18. Chemchemi yako ibarikiwe;Nawe umfurahie mke wa ujana wako.

19. Ni ayala apendaye na paa apendezaye;Maziwa yake yakutoshe sikuzote;Na kwa upendo wake ushangilie daima.

20. Mwanangu! Mbona unashangilia malaya,Na kukikumbatia kifua cha mgeni?

21. Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA,Na mienendo yake yote huitafakari.

22. Maovu yake yeye yatampata mdhalimu,Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.

Mit. 5