5. Miguu yake inatelemkia mauti;Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
6. Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari.
7. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,Wala msiache maneno ya kinywa changu.
8. Itenge njia yako mbali naye,Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
9. Usije ukawapa wengine heshima yako,Na wakorofi miaka yako;
10. Wageni wasije wakashiba nguvu zako;Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
11. Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho,Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;