1. Mwanangu, sikiliza hekima yangu;Tega sikio lako, mzisikie akili zangu;
2. Upate kuilinda busara,Na midomo yako iyahifadhi maarifa.
3. Maana midomo ya malaya hudondoza asali,Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4. Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga;Ni mkali kama upanga wa makali kuwili.
5. Miguu yake inatelemkia mauti;Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
6. Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari.
7. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,Wala msiache maneno ya kinywa changu.
8. Itenge njia yako mbali naye,Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.