8. Umtukuze, naye atakukuza;Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
9. Atakupa neema kuwa kilemba kichwani;Na kukukirimia taji ya uzuri.
10. Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu;Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11. Nimekufundisha katika njia ya hekima;Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.
12. Uendapo, hatua zako hazitadhiikika,Wala ukipiga mbio hutajikwaa.
13. Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;Mshike, maana yeye ni uzima wako.
14. Usiingie katika njia ya waovu,Wala usitembee katika njia ya wabaya.
15. Jiepushe nayo, usipite karibu nayo,Igeukie mbali, ukaende zako.
16. Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara;Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
17. Maana wao hula mkate wa uovu,Nao hunywa divai ya jeuri.