4. Naye akanifundisha, akaniambia,Moyo wako uyahifadhi maneno yangu;Shika amri zangu ukaishi.
5. Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6. Usimwache, naye atakuhifadhi;Umpende, naye atakulinda.
7. Bora hekima, basi jipatie hekima;Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
8. Umtukuze, naye atakukuza;Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
9. Atakupa neema kuwa kilemba kichwani;Na kukukirimia taji ya uzuri.
10. Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu;Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11. Nimekufundisha katika njia ya hekima;Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.
12. Uendapo, hatua zako hazitadhiikika,Wala ukipiga mbio hutajikwaa.
13. Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;Mshike, maana yeye ni uzima wako.