Mit. 4:13-22 Swahili Union Version (SUV)

13. Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;Mshike, maana yeye ni uzima wako.

14. Usiingie katika njia ya waovu,Wala usitembee katika njia ya wabaya.

15. Jiepushe nayo, usipite karibu nayo,Igeukie mbali, ukaende zako.

16. Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara;Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.

17. Maana wao hula mkate wa uovu,Nao hunywa divai ya jeuri.

18. Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo,Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.

19. Njia ya waovu ni kama giza;Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.

20. Mwanangu, sikiliza maneno yangu;Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.

21. Zisiondoke machoni pako;Uzihifadhi ndani ya moyo wako.

22. Maana ni uhai kwa wale wazipatao,Na afya ya mwili wao wote.

Mit. 4