Mit. 4:1-11 Swahili Union Version (SUV)

1. Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu,Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.

2. Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri;Msiiache sheria yangu.

3. Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu,Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.

4. Naye akanifundisha, akaniambia,Moyo wako uyahifadhi maneno yangu;Shika amri zangu ukaishi.

5. Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.

6. Usimwache, naye atakuhifadhi;Umpende, naye atakulinda.

7. Bora hekima, basi jipatie hekima;Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.

8. Umtukuze, naye atakukuza;Atakupatia heshima, ukimkumbatia.

9. Atakupa neema kuwa kilemba kichwani;Na kukukirimia taji ya uzuri.

10. Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu;Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.

11. Nimekufundisha katika njia ya hekima;Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.

Mit. 4